Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, December 21, 2013

HAWA NDIO MAWAZIRI 3 WALIOPIGWA CHINI NA RAIS JAKAYA KIKWETE, NA MMOJA ALIYEJIUZULU

Rais Jakaya Kikwete jana Ijumaa (December 20) ametengua nyadhifa za Mawaziri wanne kufuatia ripoti ya kamati iliyoundwa kuchunguza matokeo ya Operesheni Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa na wizara Maliasili na Utalii ikishirikiana wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
mawaziri
Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vua Nahodha na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mathayo David Mathayo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki aliyejiuzulu mwenyewe.
Uamuzi huo umekuja kutokana na ripoti hiyo kuonesha kuwa Operesheni Tokomeza Ujangili ilifanywa kwa unyama mkubwa wananchi mbalimbali waliteswa, kubakwa kwa wanawake na wengine kuuawa. Akitangaza hatua hiyo bungeni, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema aliongea na mawaziri hao wote wanne wakakubaliana na uamuzi huo.
“Kilichowafanya walikubali ni kwasababu moja kubwa, vyombo vilivyohusika ni vyombo ambavyo viko chini ya usimamizi wao. Hili limewapa uzito wa kuweza kusema ‘katika mazingira haya unafanyaje’,” alisema Pinda.
Mheshimiwa Pinda alisema aliongea na Rais Jakaya Kikwete ambaye amesema ameungana na wabunge waliotaka kuwajibishwa kwa wote waliohusika na uovu huo na akasema tume itakayoundwa kufanya uchunguzi itoe matokeo haraka.
“(Rais) amesisitiza sana kwamba angependa matokeo ya hiyo tume mtakayokubali kuiunda yasichukue muda mrefu na watendaji wote bila kujali ni wa ngazi gani, ilimradi kama alijiingiza katika vitendo viovu basi wawajibike kwa mujibu wa taratibu za kisheria bila kuogopa, bila kujali ili haki iweze kutendeka.”

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages