Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, December 16, 2013

PICHA: KIKWETE,KENETH KAUNDA, PRINCE CHARLES ,OPRAH WINFREY NA WAELFU WAMSINDIKIZA MANDELA KWENYE MAKAZI YAKE YA KUDUMU.

Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela Jumapili hii amezikwa kijijini kwake alikozaliwa, Qunu katika jimbo la Eastern Cape nchini Afika Kusini katika mazishi yaliyohudhuriwa na watu takriban 5,000.
Kwaheri Madiba -  Jeneza lilibeba mwili wa Mandela likiingizwa kwenye kaburi lake lililpojengwa jirani na makaburi ya wazazi wake
Kwaheri Madiba: Jeneza lilibeba mwili wa Mandela likiingizwa kwenye kaburi lake lililpojengwa jirani na makaburi ya wazazi wake
Jeneza lake lilikuwa limebebwa kwenye gari la kubebea silaha na kupelekwa kwenye makaburi ya familia. Wakati mwili wake ukiwekwa kaburini, bendera ya Afrika Kusini iliondolewa na kukabidhiwa kwa mjane Graca Machel, aliyekuwa akiliwazwa na mke wa zamani wa Mandela, Winnie Mandela.
Jeneza la Mandela likiwa limezungukwa na maafisa wa juu wa jeshi
Jeneza la Mandela likiwa limezungukwa na maafisa wa juu wa jeshi
Hata hivyo ratiba ya mazishi hayo ilizidisha muda kwa karibu masaa mawili na hivyo mila za kikabila kuwa mazishi yanatakiwa mchana wakati jua likiwa utosini ilibadilika.
Mandela alifariki December 5 akiwa na umri wa miaka 95.
Helikopta zilizobeba bendera ya Afrika Kusini juu ya kaburi la Mandela
Helikopta za kijeshi zilizokuwa zimebeba bendera za Afrika Kusini zilipita juu ya kaburi ikifuatiwa na saluti ya risasi 21

Wageni waliohudhuria ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete na marais wengine wa Afrika, Prince Charles, Oprah Winfrey, Richard Branson mwanaharakati wa Marekani, Jesse Jackson.
Oprah Winfrey (katikati) akiwa na mume wake Stedman Graham (kushoto) na bilionea wa Uingereza Richard Branson
Oprah Winfrey (katikati) akiwa na mume wake Stedman Graham (kushoto) na bilionea wa Uingereza Richard Branson
Mjukuu wa Mandela, Nand akiongea mbele ya waombolezaji huko Qunu
Mjukuu wa Mandela, Nand akiongea mbele ya waombolezaji huko Qunu
Mke wa zamani wa Mandela Winnie (kushoto) Rais Jacob Zuma na mjane wa Mandela Graca Matchel
Mke wa zamani wa Mandela Winnie (kushoto) Rais Jacob Zuma na mjane wa Mandela Graca Machel
Mtoto wa Mandela Zindzi akimliwaza muombelezaji mwingine
Mtoto wa Mandela Zindzi akimliwaza muombelezaji mwingine
Prince Charles akisalimiana na wageni wengine
Prince Charles akisalimiana na wageni wengine
Wakazi wa Qunu wakishuhudia kwa mbali mazishi
Wakazi wa Qunu wakishuhudia kwa mbali mazishi
article-2523695-1A1A0ADD00000578-769_964x676
article-2523695-1A1A8E3500000578-168_964x653
article-2523695-1A1DBD0800000578-169_964x636
article-2524000-1A1E17EF00000578-38_964x626

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages