Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 8, 2014

BAADA YA DAVIDO NA IYANYA DIAMOND ANAKUJA NA MR.FLAVOUR

Bombshell ya remix ya My Number One aliyomshirikisha Davido haimtoshi Diamond Platnumz kwakuwa bado anatarajia kudondosha nyingine. Tayari ameshafanya collabo na Iyanya huku akiipigia hesabu pia collabo nyingine na hitmaker wa ‘Nwa Baby, Mr Flavour.
                                                                               DIAMOND

Akizungumza na Capital FM jijini Dar es Salaam, Diamond amesema safari ya Nigeria imempa connection nyingi.
                                                                      MR. FLAVOUR
“Nigeria wanaitaka marker ya East Africa,” amesema Diamond ambaye video ya remix ya ‘My Number One’ imeangaliwa kwa zaidi ya 100,000 hadi sasa. “Kuna connection nyingi nimezipata nikiwa Nigeria nimefanya ngoma na Iyanya bado haijatoka itatoka baadaye. Pia nilikuwa naye amenisupport vitu vingi hata wakati na kurelease ngoma kwenye Youtube kwenye nini, amekuwa anatweet amekuwa annapost ili kuipa kiki ngoma yangu. Watu tofauti tofauti nimekutana nao ili kuangalia tufanyaje kazi pamoja,kwabababu wao ndio wameshika muziki wa Afrika kwa sasa hivi. Pia Mr flavor nina project naye.”

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages