Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 29, 2014

BILLIONAIRE AAHIDI KUTOA $120 MIL KWA MWANAUME ATAKAYE MWACHISHA BINTI YAKE USAGAJI,..MTAZAME HAPA

Bilionea wa Hong Kong, Cecil Chao bado hajakata tamaa katika jitihada zake za kumfanya binti yake aachane na usagaji na kuwa msichana wa kawaida, kiasi ambacho sasa ameamua kuongeza dau kwa mtu atakayefanikiwa kufanya kazi hiyo.
HONG KONG OUT - TAIWAN OUTThis picture taken in Macau on September 4, 2011 shows Gigi Chao (R), the daughter of Hong Kong tycoon Cecil Chao Sze-tsung with her partner.  According local September 26, 2012 reports, Cecil Chao announced a "marriage bounty" of 500 million HKD (65 million USD) to any man who can win the heart of his lesbian daughter after she married her same-sex partner of seven years in France earlier in 2012.       HONG KONG OUT - TAIWAN OUT -    AFP PHOTO/Apple Daily     ----EDITORS NOTE -- RESTRICTED TO EDITORIAL USE - MANDATORY CREDIT "AFP PHOTO/Apple Daily" - NO MARKETING NO ADVERTISING CAMPAIGNS - DISTRIBUTED AS A SERVICE TO CLIENTS - NO ARCHIVES
Gigi chao (kulia) akiwa na mpenzi wake (mwanamke) Sean Eve
Sasa atakayefanikisha kazi hiyo atapewa dola milioni 120 kwa kumgeuza msichana huyo mwenye miaka 33. Hata hivyo, Gigi Chao mwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwenzie, Sean Eve, hajaonesha dalili ama nia yoyote ya kuachana na usagaji.Na mara nyingi amekuwa akimuomba baba yake kuacha kufuatilia maisha yake.
hong-kong-cecil-chao-gigi
“Sitaki kuingilia maisha ya faragha ya mwanangu,” Cecil Chao mwenye miaka 76 ambaye anadaiwa kuwa tayari alishatembea na wanawake 10,000, aliliambia gazeti la Malaysia, Nanyang Siang Pau Jumatatu hii.”Natamani awe na ndoa njema na watoto watakaorithi biashara.”
September mwaka 2012, Chao alitengeneza vichwa vya habari pale alipotangaza zawadi ya dola milioni 60 kwa mwanaume atakayeweza kumbadilisha binti yake.
“Sidhani kama ofa ya baba yangu ya kutoa fedha inaweza kumvutia mwanaume ninayeweza,” msichana huyo ameliambia gazeti la China la Morning Post baada ya baba yake kutangaza kuongeza dau.
Gigi ni mkurugenzi kwenye kampuni ya baba yake, Cheuk Nang na hutumia muda wake mwingi kufanya kazi za kutoa misaada kama mwanzilishi wa taasisi ya Faith in Love Foundation, inayofanya kazi ya kuhimiza kujitolea katika kutokomeza umaskini. Gigi pia ni mwanzilishi wa taasisi inayotetea haki za mashoga ya Big Love Alliance.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages