Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, January 25, 2014

BOW WOW AKANUSHA KUFUKUZWA KAZI 106 & PARK.

Mashabiki wa rapper wa YMCMB, Bow Wow walipata na huzuni baada ya tetesi kuwa amepigwa chini kama mtangazaji wa kipindi maarufu cha BET, 106 & Park. Hata hivyo rapper huyo ametumia Twitter kukanusha uvumi huo.
Bow+Wow+106+Park+Tapes+in+NYC+xcoZo6fgA0Gx
Uvumi huo ulidai kuwa uongozi wa kituo hicho umemwachisha kazi Bow Wow ambaye jina lake halisi ni Shad Moss baada ya mhasibu kugundua kuwa ametumia fedha za kampuni kulipa fedha za matumizi ya mwezi ya mtoto wake aliyezaa na Joie Chavis.
vixens1694-joie-chavis
Kupitia Twitter, mtandao wa HipHopture uliamua kumuuliza rapper huyo athibitishe kwa mashabiki wake kama ni habari za ukweli.
“Clear what? That ill see yall at 6pm tomorrow live on TV like i do err day whats changed?,” Bow Wow alitweet jana.
Baadaye alitweet: In my closet at @106andpark right now doing my Ebony Magazine photo shoot. Theres some things that can be stopped, but my hustle is in motion our plan is to take over the world!”

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages