Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 29, 2014

DIAMOND APONDWA NA MASHABIKI KWA KUONEKANA NA MAMA YAKE KILA MAHALI
 Nasibu Abdul  Almaarufu kama  Diamond Plutnum ni kati ya wasanii hapa nchini ambao wamekuwa wakionyesha upendo wao wa dhati kwa mama yake  mzazi   kiasi cha kuamua kuwa naye katika maeneo mengi hata anapopata nafasi ya  kupiga show  ndani  na nje ya nchi  kitu ambacho kimeonekana  kukera baadhi ya mashabiki zake na kuhoji kuhusiana na hilo .

 Alisikika  mdau mmoja ambaye ni shabiki mkubwa sana wa msanii huyo diamond plutnum akihoji juu ya hali hiyo  nakuonekana kukereka .

“unajua wasanii wengi sana wana mama zao na kila mmoja anampenda sana mama yake mzazi kwa namna moja ama nyingine lakini kwa upande wangu mimi nahisi kama nakwazika kwa hili la Diamond , maana kila mahali anaenda na mama yake hata katika shows anazoenda kupiga za usiku  yupo na mama yake, sasa ndo kumpenda sana au ???” alihoji  shabiki huyo


mbali na huyo yupo pia mwingine aliyejitambulisha kwa jina la  Subira  Chacha  wakati akizungumza na blog hii , ambaye yupo katika manispaa ya musoma  naye alisema kitu kinachoboa zaidi ni tabia ya msanii huyo kuambatana na mama yake mzazi kila mahali.

“Diamond Plutnum ni msanii mzuri sana  maana mi mwenyewe ni shabiki wake ila ananiboa kitu kimoja tu ,tabia ya kuambatana na mama yake mzazi kila mahali, duh, inaniboa kiukweli hata kama ni upendo huo wake umepitiliza.”alisema 

Naye Blogger  Wa Blog Ya Jicho La Mdadisi na ambaye pia ni mtangazaji  wa Kituo Cha Radio Victoria  Fm 90.6 Kilichopo Musoma Mara  ,Bwana Ahmad Nandonde  katika hilo yeye alisema haina tatizo isipokuwa sio utamaduni ambao umezoeleka sana kwa hapa nyumbani ndio maana wengi wanaboreka.

“sijaona kama ni tatizo kwa  msanii huyu kuambatana na mama yake mzazi kila mahali ,lakini pia  inabidi yeye mwenyewe awe anaangalia kama ni sahihi kwa upande wake au la , na pia unajua hili wengi linawaboa lakini ni kwaajili tu haijazoeleka kwa hapa kwetu msanii kuambatana  hivyo na mama yake mzazi kila mahali na hasa katika shows zake.”alisema  Ahmadi

Diamond Plutnum  alipotafutwa kuhusianaa na hili hakuweza kupatikana  kwasababu ambazo zilielezwa kuwa ndio alikuwa anarudi hapa nchini leo hii baada ya kupiga show yake huko nchini Kenya .

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages