Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, January 16, 2014

HATIMAYE H.BABA NA DIAMOND WAMALIZA BEEF LAO YA "NATAKA KULEWA"

Jana ilikuwa siku ya kuzaliwa ya msanii wa muziki Hamis Ramadhan Baba aka H.Baba ambapo aliapa kuanza mwaka mpya na ukurasa mwingine kwa kuwasamehe wale wote waliomkosea, akiwemo Diamond Platnumz aliyemshutumu kumuibia idea yake na kuitumia kwenye wimbo wa ‘Nataka Kulewa’.
page
Akizungumza na Bongo5 jana, H.Baba aka Baba Tanzanite alisema katika kusherehekea siku hiyo muhimu ameona ni vyema asawazishe makosa yote yaliyotokea nyuma ili awe mpya.
“H.Baba ni mpya sihitaji beef sasa hivi nahitaji kufanya kazi. Diamond namheshimu na yeye ananiheshimu,kama nilimkosea mimi au alinikoea mimi tusameheane,sisi ni binadamu nimeona niyamalize ili tuishi kwa amani,” amesema muimbaji huyo.
“Tokea sakata la wizi wa nyimbo lilipotokea sema tulikuta na tukazungumza,lakini mimi imebidi niwe wa kwanza kusema kwamba hili jambo liishe kabisa. Nilizaliwa sina beef na mtu kwahiyo Nasib Abdul naomba tusameheane toka moyoni na pia kama kuna yoyote nilikosa naye naomba tusameane.”

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages