Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, January 17, 2014

HII NDIO DINI YA KANYE WEST, INAITWA "YEEZIANITY"

Kanye West amepata dini yake iitwayo Yeezianity.
Kanye-Christ
“I AM a God,” Kanye West anasikika kwenye moja ya nyimbo zake zilizopo kwenye album Yeezus (jina likiwa mchanganyiko wa aka ‘Ye – na Jesus).
Na sasa wafuasi wa rapper huyo wameanzisha website, Yeezianity.com maalum kwa watu wote wanaotaka kubadilisha dini kwenda Yeezianity, inayojitangaza kama “THE BEST CHURCH OF ALL TIME!!!!!”
Kitty Pride
“Sisi ni kundi lisilotaka kujulikana linaloamini kuwa yule anayejiita Yeezus ni kiumbe kitakatifu kilichotumwa na Mungu kuongoza kwenye kizazi kipya cha ubinadamu,” yanasomeka maneno kwenye website.
Kwenye website hiyo kuna sheria kadhaa au nguzo na tamko la imani likiwemo ‘Imani kwa Yeezus’ na ‘I believe Yeezus will lead us into a new Age of Creativity’. Amen.” Mwanzilishi wa ‘Yeezianity’ ameongea na mtandao wa Vice kwa masharti ya kutotajwa jina na kusema kuwa Yeezianity si kitu cha mzaha.
Ingia hapa kusoma website ya dini hiyo.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages