Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, January 14, 2014

PICHA: DIAMOND,PROFESA JAY NA P FUNK WAKIWA STUDIO,..INAWEZEKANA WANAPIKA KITU?!!

Unapata picha gani pale the heavyweight MC anapokutana na ‘the Bongo Flava Prince’kwenye wimbo uliotayarishwa na ‘Godfather wa Bongo Flava’.. Kwa wengi mchanganyiko huo unatoa mnuso mzuri wa hit ya mwaka.
Bd63dmqIMAA6FlH.jpg large
Basi ndicho kilichofanyika, Profesa Jay amemshirikisha Diamond Platnumz kwenye wimbo wake mpya unaotayarishwa na producer wa Bongo Records, P-Funk Majani.
Wimbo huu utakuwa wa kihistoria hasa kwakuwa ni kazi iliyowakutanisha Profesa na P-Funk baada ya miaka mingi ya kutofanya kazi pamoja. Majani anabeba sifa zote za kumtengeneza Profesa Jay huyu ambaye kwa wengi anapewa heshima ya kuwa rapper anayeheshimika zaidi kwenye historia ya muziki wa Bongo Flava.
Majani ndiye aliyekuwa kichwa nyuma ya hit za Jay zikiwemo Jina Langu, Ndio Mzee, Zali la Mentali, Nikusaidieje na zingine kibao kwenye album ya mwaka 2001, Machozi, Jasho na Damu. Sina shaka kuwa ujio wao mpya utakuwa wa kishindo.
Sababu ya pili kubwa ya kwanini collabo hii itakuwa ya mwaka, ni uwepo wa Diamond Platnumz ambaye yupo katika kilele cha mafanikio huku akiwa amejikusanyia mashabiki wengi kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na sasa hadi nchi zingine nyingi za Afrika kutokana na collabo yake na Davido wa Nigeria.
Profesa Jay ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule amepost picha kwenye Instagram akiwa na wawili hao kwenye studio mpya za Bongo Records na kuandika: Studio session at Bongo Records with the Super dupa producer P – Funk and Diamond Platnumz himself COOKING for all yall!! Stay Tuned.”
We can’t wait..

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages