Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, January 10, 2014

YAYA TOURE ASHINDA TENA KWA MARAYA TATU TUZO YA MCHEZAJI BORA BARANI AFRIKA

Yaya Touré, kiungo wa Ivory Coast, amechaguliwa kwa mara ya tatu kama mchezaji bora wa mwaka barani Afrika.Mchezaji huyo wa Manchester City amewashinda Mikel John Obi wa Nigeria na mwenzie wa Ivory Coast Didier Drogba.
“Najivunia na ni mwenye furaha kuwa mshindi leo,” Touré, aliyekuwa amevalia nguo za tamaduni ya Nigerian aliwaambia waliohudhuria hafla hiyo mjini Lagos. “Nampongeza kaka yangu Obi Mikel aliyekuwa akistahili pia.”
Mchezaji huyo ameshinda baada ya kupigiwa kura na makocha wa timu za taifa za Afrika. Abedi Pele wa Ghana alishinda tuzo hiyo kwa mara tatu mfululizo kuanzia 1991–93 wakati mchezaji wa Cameroon Samuel Eto’o akishinda kuanzia 2003-05 na kushinda tena mwaka 2010

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages