Breaking

Post Top Ad

Monday, January 6, 2014

VIDEO: YASINTA TALLY, MWANADADA ANAEWAKILISHA MWANZA VYEMA KWA UPANDE WA HIPHOP.

Jiji la mwanza linasifika sana kwa kutoa vipaji vingi vinavyowakilisha mziki wa Hiphop, baadhi ya wasanii waliotokea mwanza na wanafanya poa sana ni Fid Q, Young Killer, Kala Jeremiah na wengine wengi.

Ukweli ni kwamba wasanii wote nliowataja hapo juu ni wa jinsia moja yani wa kiume. Kumekua na uchache wa wadada wanaofanya mziki wa Hiphop mkoani mwanza. Admin wenu nikiwa likizo mwishoni mwa mwaka jana jijini mwanza na ndipo nlipokutana na mwanadada Yasinta Tally.

Yasinta ni mwanadada anayefanya mziki wa Hiphop na anawakilisha vyema pande za Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla. Yasinta ana uwezo wa kuflow kwa lugha mbili tofauti yani kingereza na kiswahili. Na style yake ni ya tofauti kidogo kitu ambacho naamini akipata nafasi ataiwakilisha vyema tanzania na hata nje ya nchi atafanya poa.

Unaweza itazama video mpya ya Yasinta aliyomshirikisha Fred Swag, video inakwenda kwa jina la Feel Me Today hapa chini

Post Top Ad

Pages