BABY MADAHA : "SHILOLE NI MCHEZA VIGODORO"


MSANII wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Madaha’ amemchana staa mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kwa kumwambia ni mcheza muziki wa uswahilini (vigodoro).

Kauli hiyo ya msanii huyo anayetamba na Wimbo wa Summer Holyday, ameitoa siku chache baada Shilole kutema cheche zake kuwa Madaha aache kumfuatilia kwani amekuwa akiingia kwenye anga zake mara kwa mara.

“Hivi huyu ana akili au matope, nimfuatefuate ana nini? Hebu aangalie muziki wangu ninaopiga na wake. Yeye ni wa hapa hapa, mcheza vigodoro,” alifunguka Madaha

0 comments:

linkwithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...