Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, February 24, 2014

HATIMAYE HUDDAH MONROE AMTANGAZA MOUSTAPHA COLONEL KUWA NI MPENZI WAKE MPYA.

Huddah Monroe na Moustapha Colonel si marafiki tu, ni wapenzi. Wakiongea na kituo cha KTN, mastaa hao wamedai kuwa siku za hivi karibuni wamekuwa na ukaribu kiasi cha kuingia studio na kufanya wimbo pamoja.
huddah
“Nampenda kwa kweli kama rafiki yangu, tumefanya project naye, tumeenda kwenye studio, tumefanya ngoma naye so katika kupatana, we are just looking for the next step,” alisema Huddah.
Hata hivyo mastaa hao waliokuwa wakiongea kwa kujiumauma hasa katika kuthibitisha uhusiano wao, wamesema uhusiano huo si wa kutafuta umaarufu ambapo Moustapha alidai kuwa Prezzo alikuwa akimchezea tu Huddah ambaye kwake ni msichana wa kipekee.

“Sijui kwanini alimtesa msichana mzuri kama huyu, msichana yaani watu wanavyomchukulia huko nje ni tofauti kabisa,”alisema Moustapha. “Huddah ni mzuri, mtoto mzuri. Kama kuna mwanamke mzuri kushinda Huddah hivi sasa tunavyoongea itakuwa tatizo sana,” alisema Moustapha kujibu swali la kwanini ameamua kumchagua Huddah na kudai kuwa haikuwa rahisi kumpata.
Moustapha amesema hata mama yake mzazi amemkubali Huddah kuwa mchumba wake.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages