Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, February 1, 2014

TAZAMA JOKATE ALIVYO-MSURPRISE WEMA STEGINI KWA KUMWAGIA MINOTI YA MAANA WAKATI WA SHOO YA MIRROR ARUSHA.IMG-20140202-WA0012

Unaweza kujikuta ukishindwa kuielewa hii hali lakini inabidi ukubaliane na ukweli halisi wa hiki kilichotokea,Jokate na Wema historia yao ilianzia kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo Mshindi alikua ni Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa Lissa Jensen.
2006

Headline zilikuja kutengenezwa tena zikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako na mtu mmoja ambapo magazeti mengi yaliandika mahusiano haya  yaliyokua yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na warembo hawa.
IMG-20140202-WA0009

Kimepita kimya kirefu sana juu ya hawa watu wawili hadi usiku wa February 01 huko Arusha kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame ambalo ndani yake kulikua na mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid Benzi,Mirror,Jordan na wengine kibao.
IMG-20140202-WA0011
Wakati Madam Wema Sepetu akimwaga mauno kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu yoyote Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza Wema pesa na wakati huo Wema alikua akicheza Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’ ambapo Jokate aliungana na Wema kuucheza Wimbo huo.
IMG-20140202-WA0008


Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages