Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, March 10, 2014

JAY Z AKUBALI KUWA "BEST MAN" WA NDOA YA KANYE WEST, NDOA ITAKAYOFANYIKA MAY MWAKA HUU


Jay-Z amekubali kuwa best friend wa Kanye West katika sherehe za ndoa ya swahiba wake huyo na mwanamitindo Kim Kardashian itakayofanyika May mwaka huu lakini ametoa masharti ya kutooneshwa kwenye kituo chochote cha runinga.
“Jay Z amekubali katika hatua za awali lakini ametoa sharti moja kuwa katika hali yoyote yeye, mkewe Beyonce na mtoto wao Blue Ivy wasioneshwe kwenye runinga katika sherehe hizo.” Mtu wa karibu wa Kim Kardashian ameiambia Daily Star.
Hata hivyo huu unaonekana utakuwa mtihani kwa Kanye West na Kim Kardshian kwa kuwa kituo cha runinga cha E! kitalipa mkwanja mrefu kwa ajili ya kuonesha ndoa hiyo itakayofanyika Paris, Ufaransa.
Na hiyo ingekuwa faida kwa reality show ya familia ya Kim Kardashian ‘Keep Up with The Kardashians’ kwa kuwa ingeteka watazamaji wengi duniani kufuatia tukio hilo.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages