Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 21, 2014

OPRAH AANZISHA MAJANI YAKE YA CHAI,.YENYE JINA LA KISWAHILI "OPRAH CHAI"

Malkia wa talk show Oprah Winfrey ameingia katika biashara mpya ya majani ya chai ambayo ameyaita jina la Kiswahili ‘Oprah Chai’.
Howard Schultz announces the new Teavana Oprah Chai Tea with Oprah Winfrey during the company's annual shareholders meeting in Seattle
Oprah Winfrey na Howard Schultz
Oprah ameungana na rafiki yake bilionea Howard Schultz wa kampuni ya Starbucks katika kuanzisha mradi huo wa majani ya chai, ambao umetangazwa Jumatano ya wiki hii wakati wa mkutano wa kila mwaka wa kampuni hiyo.
oprah chai-2
Majani hayo ya ‘Oprah Chai’ yatapatikana katika ladha mbalimbali ikiwemo ya mdalasini, tangawizi, iliki pamoja na karafuu.
Katika kila bidhaa ya ‘Oprah Chai’ itakayouzwa, kampuni iliyoingia ubia na Oprah ya Starbucks itatoa mchango kwa shule ya wasichana iitwayo ‘Oprah Winfrey Leadership Academy’ iliyoianzishwa na inayofadhiliwa na Oprah, iliyoko nchini Afrika Kusini.
Oprah Chai itaingia sokoni (April 29) huko Marekani na Canada.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages