Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, March 6, 2014

TAZAMA HAPA VIDEO NA PICHA YA YULE CHATU ALIYE MMEZA MAMBA "WALIPIGANA KWA MASAA MATANO"

 Nyoka anapommeza mamba si jambo la kawaida. Huko Australia, Jumapili iliyopita, wananchi walishuhudia sinema ya bure iliyochukua muda wa saa tano kati ya chatu mkubwa mwenye urefu wa futi 10 na mamba mwenye urefu wa mita moja na picha lote likarekodiwa kwenye kamera.

Tiffany Corlis, mwandishi wa habari wa Australia, alipiga picha tukio hilo.
SB-snake_gall13-20140303141439466626-600x400
Chatu akimmeza mamba
Kwenye mahojiano na The Sydney Morning Herald, Tiffany Corlis anasema timbwili hilo lilitokea kwenye ziwa Moondarra huko Queensland, Australia, wakati yeye akipata chai na wavuvi kumpa taarifa kuwa kulikuwa na vita kati ya joka na mamba huyo.
nyoka10
Mamba aliyekuwa amekufa tayari akiishilia tumboni mwa chatu mwenye futi 10

Kwa mujibu ya watu hao, vita hivyo kati ya nyoka huyo wa majini na mamba ilianza kwenye maji wakati mamba alipokuwa akijaribu kukitoa kichwa chake nje ya maji ili apone. Mpaka muda ambapo Tiffany Corlis aliweza kuchukua picha, nyoka huyo alikuwa tayari amejivilingisha kwenye umbo hilo kumbana.
nyoka6
nyoka8
Mamba akiwa amebanwa vyema na chatu
“It was amazing. We saw the snake fighting with the crocodile – it would roll the crocodile around to get a better grip, and coil its body around the crocodile’s legs to hold it tight. After the crocodile had died, the snake uncoiled itself, came around to the front, and started to eat the crocodile, face-first.”
Shuhuda mwingine alisema vita hiyo ilichukua muda wa saa tano na hadi muda huo wote walionekana kuchoka.
nyoka5
nyoka7
Baada ya hapo nyoka huyo alimmeza mamba huku watu hao wakishuhudia
Tiffany Corlis anadai ilimchukua nyoka huyo takriban dakika 15 kummeza kabisa mamba huyo. “Nyoka alikuwa amejaa kabisa baada ya kumaliza. Sijui alienda wapi baada ya hapo, wote tuliondoka hatukataka kuendelea kuwepo.”
nyoka14
nyoka12
nyoka11
nyoka4
nyoka3
nyoka2
nyoka1

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages