Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, May 15, 2014

HIKI NDICHO KISA CHA SOLANGE KUMPIGA SHEMEJI YAKE JAYZ. SOMA HAPA.

Wapashaji wa habari za udaku na umbeya hawalali wakitafuta chanzo cha Solange kugeuka kama mbogo aliyejeruhiwa na kumshambulia shemeji yake, Jay Z mbele ya dada yake Beyonce aliyeamua kukaa pembeni kuwaangalia asifanye kitu.
jay-z-beyonce-solange-met-gala-fight-billboard-650
TMZ walipata kipande cha video kilichoonesha tukio hilo zima lililotokea kwenye lifti ya hoteli huko jijini New York, Marekani ambapo watatu hao walikuwa wanatoka kwenye after party ya Met Gala.
Na sasa mtandao wa Perez Hilton umedai kupata habari mpya za kile kinachoweza kuwa sababu ya mdogo wake Beyoncé kumpiga ngumi na mateke Jigga na kumuongezea tatizo la 100!! Inasemekana kuwa picha lilianza baada ya Solange kuwaalika marafiki zake kadhaa ambao sio maarufu kwenye party hiyo. Wageni hao wanadaiwa kuzungumza kauli zilizomkera Jay Z.
Solange alitaka kuondoka kwenye party hiyo lakini wakati anaondoka, Jay alidai kuwa angepita kwenye party ya Rihanna ya Up & Down peke yake. Baada ya Solange kubaini kuwa Jay angehudhuria party hiyo peke yake, ndipo Solange akamind.
“Alionekana kuwa amelewa na kukasirika. Alisema ‘Kwanini usiende nyumbani’ na akamwambia Beyonce ‘Kwanini mume wako anahitaji kwenda club sasa?’” Jay anadaiwa kutonyamaza na kumtuhumu Solange kuwa ni mama mbaya ambaye hujirusha mara nyingi na ndipo Solange alipoanza kumshambulia.
Mwisho wa siku Jay aliamua kutoenda kwenye party ya Rihanna.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages