Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 27, 2014

MWIGIZAJI BONGO MOVIE RECHO HAULE AIAGA DUNIA, WAKATI AKIJIFUNGUA. NA MTOTO AFARIKI PIA.

Kiwanda cha filamu nchini, kimepata pigo jingine baada ya kuondokewa na muigizaji na mtayarishaji wa filamu wa kike aliyekuwa anakuja juu, Rachel Haule. Rachel amefariki jana baada ya kujifungua kwa upasuaji.
Rechal-Haule-540
“Kiufupi rachel alikuwa mjamzito… Na taarifa niliyoipata tangu jana ni kwamba kulitokea complications wakati wa kujifungua ambapo alijifungua kwa operation mtoto akafariki na yeye akawa amelazwa icu.. Lakini asubuhi ya leo mungu akamchukua na yeye…. Hivyo ni mama na mtoto ambao wamepotea.. Pole sana Saguda kwa msiba huu mkubwa wa kupoteza mama na mtoto,!!!!! Kazi ya mungu haina makosa,” ameandika Zamaradi Mketema kwenye Instagram.
“Jana alifanikiwa kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya uzazi baada ya hapo hali yake haikuwa nzuri aliwekwa katika chumba cha wagojwa mahututi, kwa bahati mbaya leo asubuhi ameaga dunia,”rafiki yake wa karibu aliuambia mtandao wa Filamu Central.
Rachel aliigiza kwenye filamu mbalimbali zikiwemo Vanessa in Dillema na Men’s Day Out. Kifo chake kimekuja siku chache baada ya muongozaji na muigizaji wa filamu Adam Kuambiana kufariki dunia. Msiba huo umepokelewa kwa majonzi na mastaa mbalimbali nchini.
Shilole
Staki kumkufur mwenyez Mungu wangu! Ila kazi yake haina makosa tulimpenda ila mwenyezi Mungu kampenda zaid! Dah inauma sana pole Saguda kwa mtihan uliokupata!Ila tupo pamoja kwa kipind hik kigumu 1h

Zamaradi Mketema

OMG!!! Sijawahi kushtuka kama hivi… nasikitika kutangaza MSIBA mwingine mkubwa ndani ya BONGO MOVIE!!! RACHEL HAULE hatunae tena duniani… AMEFARIKI Asubuhi ya leo… INALILLAHI WAINAILAIHI RAJIUN…. pumzika kwa Amani mama… MUNGU YUPO jamani!!!!! 2h
Jacky Wolper
Recho haule me nakutambua kma sheilah kipnd ni rafk yangu kipenz nilikua napenda kukuita sheila .R.i.p sheilah umeamua kumzalia mwanaume unaempenda saguda lkn aikufanikiwa mtoto akaiga dunia na sasa umefwata wewe jaman ni pigo kubwa kwakijana yule na kwa famly na sisi bongo movie pia..Mungu amekupenda zaidi ..pole saguda shemeji yetu…R.I.P sheilah 8min
Riyamaally
Innalilahi wainna ilaihirajiun mbele yako nyuma yetu kazi ya mungu hainamakosa kila nafsi itaonja umauti mungu akuweke unapo stahili maa amen daima tutakukumbuka na pengo lako halitafutika kamwe pumzika kwa amani pole sana kaka saguda mungu akujalie sunira na uvumilivu amin pole familia pole bongo muvi na tuwe pole kwa sote kila alie guswa na msiba huu jamaa na marafiki ,,,,natue pole kwa sote kazi yake mola daima haina makosa mungu ameleta nae amechukua jina lake lihimiliwe milele amin 5min
Barnaba Elias
ROHOO inaniuma uwiii Bongo movie jamani mungu Tusamehe kabla aujatuonesha mwisho wetu mana we Uwa unakuja Bila hod wala Taharifa na kazi yako amna mtu ambaye anakuzuiya tupe moyo wa kufanya kaz yako na kutukumbisha huyapendayo Amina jamani Huyu dada nilikuwa napenda sana kaz zake naye ameenda jamani Amefariki Leo asubuhi kwenye Hosptali ya mwimbili na kwa bahati mbaya alijifungua Mtoto kwa bahati mbaya Mtoto amefariki na yeye mwenyewe pia jamani polen Bongo movie pole Team yenu yote !!!!! Anaitwa RECHO….!! 7min
Read more at http://web.stagram.com/feed/#CGBdSQpwu2XeoqUo.99

Batulli

batuli_actress Alhamdulilah……Innalilah Wainnailah Rajouun “Yarabbi Tupe Subira, Yarabbi Tupe Uvumilivu

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages