Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, August 18, 2014

ALICHOKISEMA BABU TALE KATIKA KUSIMAMIA KAZI ZA DIAMOND. SOMA HAPA

Diamond Platnumz ni msanii mkubwa Tanzania na hata nje kwa sasa, na kazi kubwa ya usimamizi wa kazi zake inafanywa na timu inayoongozwa na meneja wake Babu Tale anayeshirikiana na Said Fella pamoja na watu wengine.
babu-tale
Mara nyingi mashabiki hua wanaona mafanikio ya msanii baada ya kupatikana kwa mafanikio hayo, lakini hawajui ni ugumu gani ambao timu inayokuwa nyuma ya msanii huyo inakutana nao katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.
Kupitia kipindi cha Sunrise cha Times FM, Ijumaa iliyopita Babu Tale aligusia kwa ufupi ugumu anaokutana nao katika kumsimamia msanii mkubwa kama Diamond, baada ya kuulizwa ni ugumu gani anaokutana nao kumsimamia msanii mkubwa.
“Ni stress…ni stress kubwa asikwambie mtu yaani kum’manage’ msanii mkubwa ni stress kubwa, “ alisisitiza Babu Tale ambaye pia ni meneja wa Tip Top Connection.
“Sio tu kwenye muziki sometimes hata mambo ya family, sometimes unakutana na msanii wako amepost kitu ambacho huna tension nacho unashtuka, sababu sikuhizi sifanyi interview nyumbani tu, nafanya interview East Africa, West Africa, South Africa zile media kubwa za nje, sometimes hata Diamond akiandika Kiswahili unaona mtu wa nje anaomba kuuliza ameandika nini ili nae aondoke na ile story.”
Aliendelea,
“Inakujia wakati mgumu, yet Diamond ni binadamu kama ulivyokuwa wewe kama nilivyokuwa mimi, ana feelings zake za kibinadamu pia. Anapokuwa anatamani kupost kitu ambacho kinahusiana na hisia zake, haihusiani na kazi yangu mimi na yeye, pia inaniathiri mimi, lakini mwisho wa siku natakiwa nimuelewe kama yule ni binadamu ambaye ameamua kutoa lake la kibinadamu naliacha kama lilivyo.”
Tale alimalizia,
“Sometimes hata media watu kutaka kufanya interview na Diamond mwingine analaumu bana mimi Diamond simpati kwenye simu au namwita kwenye interview haji. Diamond anaishi kwa kutegemea media anaishi kwa kutegemea mashabiki wake, hakuna msanii anayekata kufanya interview kama anajua hii ndio inaniweka sehemu nzuri. Ila sometimes vitu vinavyosongana katika kazi zinachangia…Babu Tale hebu ongea nao. Hizo ni changamoto za kumsimamia msanii mkubwa.”

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages