Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, September 17, 2014

ALICHOKISEMA NUH MZIWANDA BAADA YA KUKATALIWA UKWENI KWA KINA SHILOLE. SOMA HAPA


Tukio hilo lilijiri ndani ya Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini hapa wakati wawili hao walipokuwa wakipafomu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta ndipo mashabiki waliposema hawamkubali Nuh na badala yake aolewe na DJ Zirro.
Wakati shoo ya wawili hao ikiendelea, Shilole alikatisha muziki kwa muda na kuwaambia mashabiki kupitia kipaza sauti wamwambie kama Nuh Mziwanda ana vigezo vya kuwa mumewe ndipo wakasema hapana na kumpendekeza DJ Zirro ambaye alikuwa akipiga muziki kwenye shoo hiyo.
Staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’, akiwa na mpenzi wake Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’.
“Hatumtaki Nuh Mziwanda awe shemeji yetu, bora uolewe na DJ Zirro. Sisi ndiyo tumeamua hivyo,” alisikika mmoja wa mashabiki waliokuwa wakifuatilia burudani hiyo.
Kitendo hicho cha mashabiki kumkataa Nuh Mziwanda kilimfanya bwa’mdogo huyo ambaye naye anaimba muziki wa Bongo Fleva kujikuta akiropoka na kusema:“Kama mnadhani sina hela basi naomba nitoe mahari hapahapa,” alisema Nuh huku akiwatupia mashabiki kiasi kidogo cha fedha.
Pamoja na kufanya hivyo, bado mashabiki waliendelea kumkataa Nuh Mziwanda hadi aliposhuka jukwaani ambapo alionekana kukwazwa na jambo hilo kwani tokea aliposhuka alikosa raha kabisa.
Paparazi wetu alimfuata Nuh Mziwanda alipokuwa ameketi baada ya kushuka jukwaani na kumuuliza amejisikiaje kukataliwa ukweni, akafunguka:
Staa wa Mduara Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shishi Baby’,
“Kusema kweli kuna muda nimejisikia vibaya ingawa hapohapo jukwaani nilijifikiria na kugundua kuwa ni gemu tu hivyo nimejifariji kwa kuona kama ni sehemu ya burudani tu,” alisema Nuh Mziwanda

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages