Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 12, 2014

PICHA: OSCAR PISTORIUS AHUKUMIWA KWA KUUA BILA KUKUSUDIWA. TAZAMA ILIVYOKUWA HAPO MAHAKAMANI.

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius.
MWANARIADHA mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amepatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa bahati mbaya.

Oscar Pistorius akisikiliza hukumu yake.
Akitoa uamuzi wake, Jaji Thokozile Masipaa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya alipofyatua risasi kupitia kwa mlango wake wa choo akiwa katika hali ya mshtuko akidhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Baba mzazi wa Oscar, Henke Pistorius akifuatilia kwa makini hukumu ya kijana wake.
Alisema kuwa upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha kuwa Pistorius alinuia kumuua Steenkamp na kutekeleza mauaji hayo kwa kusudi.

Wanafamilia kutoka uoande wa marehemu Reeva wakiwa na simanzi wakati wa hukumu hiyo.
Pia alipatikana na hatia ya kosa la kutumia silaha yake visivyo alipokwenda mgahawani.
Adhabu yake itatolewa Oktoba 13 mwaka huu.
Jaji Thokozile Masipa alisema kuwa mwanariadha huyo alimuua Reeva kwa bahati mbaya.
Dada wa Pistorius, Aimee (katikati) akisikiliza hukumu ya kaka yake.
(CREDIT: BBC)

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages