Breaking

Post Top Ad

Monday, November 17, 2014

SOMA HII: MASAI HUYU AMPOSA WEMA,..APELEKA BARUA YA UCHUMBA KWA MAMA WEMA SEPETU.


GOOD news? Habari mpya kutoka kwa mlimbwende asiyechuja Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam au Beautiful Onyinye’ ni kwamba, Mmasai wa Kigoma, Ayoub Nyembo ‘Masai’ ameibuka na kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwa wazazi wa mrembo huyo, Sinza-Mori jijini Dar, Ijumaa Wikienda lina mkanda mzima.

WAZO LILIVYOIBUKA

Mtu wa karibu na Masai alilipenyezea gazeti hili habari kuwa, baada ya habari za Wema kummwaga mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuandikwa magazetini hivi karibuni, fasta Masai aliiona fursa ‘u-single’ kwa Wema, akatangaza nia ya kumposa kwani alikuwa akimzimia muda mrefu.

“Masai ametumia fursa, hakutaka kuchelewa maana wazo alikuwa nalo kitambo lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kumhofia Diamond,” alisema mtu huyo.


AKUTANISHWA NA IJUMAA WIKIENDA

Baada ya mtu huyo wa karibu na Masai kupata mawasiliano ya Ijumaa Wikienda kisha alikutanishwa nalo maeneo ya Mwenge jijini Dar akiwa tayari ‘amejikoki’, mkononi akiwa na barua ya uchumba sambamba na bahasha yenye shilingi elfu hamsini kama posa.


Ijumaa Wikienda: Unataka kumuoa Wema kweli au unazingua?

Masai: Nipo ‘serious’ ndiyo maana unaona nimekuja kwako nikiwa kamili na mshenga wangu nipeleke kwa mama Wema.


SAFARI KWA MAMA WEMA

Huku mwanahabari wetu akigonga picha za kumwaga kwa kila hatua, alimwelekeza Masai huyo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva nyumbani kwa mama Wema, Mariam Sepetu ‘Mkwe’ ambapo waliambatana na mshenga wake lakini walipokaribia, Masai alikaa sehemu na kumtuma mshenga azame ndani.


NDANI KWA MZAA CHEMA

Mshenga alipozama ndani, alikutana na mfanyakazi wa ndani (house girl) ambaye alipokea barua hiyo ya uchumba na kumpelekea moja kwa moja mama Wema.


BARUA YASOMWA

Baada ya kutua mikononi mwa mama Wema, aliisoma barua ya uchumba kisha akamuomba mshenga kuingia ndani huku akiwa na furaha hususan pale alipogundua kuwa mkwewe mtarajiwa (Masai) ni mtu wa Kigoma.


MAZUNGUMZO YA FURAHA 

“Kwa hiyo Wema wangu anatakiwa aolewe Kigoma akale migebuka eeh?,” mama alimuuliza mshenga.


Bila hiyana mshenga akajibu: “Ndiyo mama, Masai anaishi Kigoma ila ana nyumba zake Dar, huwa anakuja mara kwa mara kwenye biashara zake na pia ana mji Singida katika Kijiji cha Ikungi na ni mfugaji mzuri, ng’ombe anao wa kutosha.”Shangwe zaidi iliongezeka kwa mama Wema baada ya kusikia Masai huyo ana mji Singida tena kwenye kijiji ambacho yeye anatokea akatoa masharti kuwa afuate taratibu za Kitanzania kwa kumtaka Masai azungumze na Wema kisha ampigie simu ndiyo apokee barua kwa amani.


HUYU HAPA MAMA WEMA

“Hili ni jambo la kheri jamani, nimekuelewa lakini uchukue barua hii sambamba na posa urudi kwanza ukamwambie huyo mkwe mtarajiwa azungumze na Wema wakikubaliana, Wema yeye ndiye aniambie siku ya ninyi kuja kutoa posa ili na mimi nijiandae,” alisema mama Wema.

  CHANZO  :Globalpublishers

Post Top Ad

Pages