Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, December 19, 2014

DIAMOND PLATNUMZ: HII NDIO SABABU ILIYONIFANYA NIACHANE NA PENNY. SOMA ZAIDI HAPA

Diamond Platnumz amedai kisa cha kumuacha mpenzi wake wa zamani, Penny ni mrembo huyo kutoa mimba zake.
MONDNAPENY
Muimbaji huyo wa Ntampata Wapi ameiambia Global TV kuwa alipewa sababu ya kutolewa kwa mimba hizo lakini hakuridhika nayo na kudai kuwa story ilikuwa na ubabaishaji mwingi.
“Mjini kuna mambo mengi sana, ” alisema. “Unaweza ukawa na mwanamke ana mimba yako from nowhere akaitoa tu, akajisikia akaitoa na sitaki kuwa na mwanamke nikaoneka ninam-force tuzae. Mwingine anaweza akajua unataka kumharibia ujana wake. Zile sehemu zote nilizopita pita nilishaligusiaga lile suala nikaona napigwa chenga ndio maana sometimes hunielewi nimepita huku nimetokea huku,” aliongeza.
“Mjini ujanja ujanja mwingi, ndio maana umesikia niliachana na Penny na Penny nilimnunulia gari na sijawahi kumwambia chochote yaani. Mimi mwenyewe naamini hakuwahi kuamini huko aliko nikachulia barida tu! Na kweli aliwahi kuwa na ujauzito wangu na baada ya kuniambia ana ujauzito wangu nikampeleka mwenyewe nikaupima papu nikaona huu hapa! Asubuhi tu nikamtia ndinga ‘tulia mimi nataka kababy! From nowhere sijui nini sababu za uongo na kweli ikaja ikatolewa, naomba sababu sipewi ya msingi. Naambiwa ‘ooh sijui home sijui nini!
Nilijisikia vibaya kama binadamu nikaona poa, sikutaka kuleta uswahili fresh tu! Nikagonga kengine, hii pia kikatolewa. Nikaona miyeyusho ndo hapo mahusiano yetu yalikufa.”
Bongo5 ilimtafuta Penny ambaye alisema alishafunga ukurasa wa kuongelea mambo ya ex wake huyo.
Penny1
“Mimi habari za Diamond niliacha kuongelea, habari za Diamond nimemaliza sasa mimi nina ukurasa wangu kabisa, ” alisisitiza.
“Miaka miwili nilikuwa naongea habari ya Diamond nimechoka! Tuhuma zote alizonituhumu Diamond mimi nataka anituhumu mpaka anakufa, mimi siwezi kujibu chochote. Sitaki kumuongelea Diamond.”

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages