Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, January 24, 2015

FINALLY!! WEMA SEPETU KAONGEA ISHU YA KUMPELEKA DIAMOND POLISI,.. SOMA HAPA


Baada ya hapo jana meneja wa mwigizaji Wema Sepetu, Martin Kadinda  kukanusha habari za Wema kumpeleka polisi Diamond Platnumz ambae alikuwa mpezi wake. Kwa kutoweza kulipa kwa wakati deni la shilingi million 10. Leo Wema Sepetu amefunguka  kuhusu swala hili katika mahojiano na Millard Ayo.

Wema  ameyasema haya “Hii taarifa imenishtua sana maana asubuhi ya jana nimekuta kwenye gazeti wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa sababu muda mwingi siendeshi mimi akaunti yangu ya twitter, anaiendesha mtu wangu wa blog Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko“

Nilishasema ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia tena, nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa kila kitu ili kuepuka haya maneno

 “Hakuna kitu ambacho namdai Diamond,hakuna siku hata moja nimefikiria kwenda kumshtaki Diamond labda kama kungekuwa kuna kitu chochote, yaani labda kungekuwa na ukweli wa kitu chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda polisi, sijawahi kufanya kitu cha namna hii hizi taarifa zimenishtua sana

Sijawahi kujiunga VICOBA maana sivijui, nilikua nimekaa na mtu akanambia labda Wema hujui  hawa watu wa VICOBA wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na kutengeneza hii kitu kwamba VICOBA wanaweza kukopa hadi Milioni kumi… kwanza mimi siwezi kukopa Milioni 10..“– Wema Sepetu.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages