Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, January 14, 2015

MNYAMA!!! SIMBA YATWAA KOMBE LA MAPINDUZI.. YAICHAKAZA MTIBWA SUGAR

Simba Bingwaaaa_full
DSC04969Dakika ya 63 beki wa kulia wa Simba, Hassan Ramadhan Kessy aliachia shuti kali lililogonga mwamba na kuingia tena uwanjani.
Hajib alikwenda kumuona tena kipa Mohammed, lakini alishindwa kutumia vyema pasi ya Ramadhan Singano ‘Messi’ kufuatia kipa huyo wa zamani wa Yanga kuudaka mpira.
Kocha Kopunovic alifanya mabadiliko katika dakika ya 65 akimtoa Hajibu na nafasi yake kuchukuliwa na Elius Mguli.
Kuingia kwa Maguli kuliongeza kasi ya Simba katika safu ya ushambuliaji.
Katika dakika ya 65, Mtibwa walimtoa Musa Nampaka na nafasi yake kuchukuliwa na Ibrahim Rajab.
Dakika ya 75 Emmanuel Okwi alikwenda benchi nafasi yake ikachukuliwa na Awadh Juma.
Musa Hassan Mgosi alioneshwa kadi ya njano katika dakika ya 78 kufautia kumchezea vibaya Kessy.
Dakika ya 87 Mtibwa walimtoa Ally Shomari na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhan Kichuya.
Dakika ya 89 Simba walimtoa Ndemla na nafasi yake kuchukuliwa na Shaaban Kisiga.
Katika dakika ya 90 Mtibwa Sugar walimtoa Ame Ally na nafasi yake kuchukuliwa na Abdallah Juma.
Kuhakikisha wanatwaa ubingwa, Simba walimtoa Peter Manyika katika dakika ya 90 na nafasi yake kuchukuliwa na Ivo Mapunda.
Mapunda ni mzoefu wa kudaka penalti hakuwaangusha katika mapigo hayo.
Mpaka dakika 90 zinamalizika, hakuna timu iliyoona lango la mwenzako.
Baada ya hapo mikwaju ya penalti ilifuata na Simba ndio walikuwa wa kwanza kupiga.
Waliofunga Penalti kwa upande wa Simba ni Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Danny Sserunkuma wakati Shaaban Kisiga alikosa.
Waliofunga kwa upande wa Mtibwa Sugar ni Ally Lundenga, Shaaban Nditi, , Ramadhan Kichuya, wakati Ibrahim Rajab na Vicent Barnabas walikosa penalti hizo.
???????????????????????????????
???????????????????????????????
???????????????????????????????

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages