Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 26, 2015

HATIMAYE CHID BENZ AACHIWA HURU BAADA YA FAINI YA SH LAKI 9. MSIKILIZE HAPA AKIONGEA.

Chidi Benz aachiwa huru baada ya kulipa faini ya shilingi laki 9

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia huru mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 au kwenda jela miaka miwili kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya, ambapo amefanikiwaa kulipa pesa hizo na kuachiwa huru.
Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.Chidi Benz alikiri kosa hilo wiki iliyopita, mbele ya mahakama ya kisutu kuwa alikamatwa uwanjani hapo na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi 38,000 na bangi yenye thamani ya ashilingi 1,700, pamoja na vifaa vya kuvutia ambavyo ni kigae na kijiko, akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.akizungumza na Clouds Fm ndani ya xxl live leo hii, Chidi amesema:
"Nimejifunza kwasababu kuna maisha halisi ambayo mimi nimeyaishi kati kati hapo, matatizo na kwenye maisha mi naona yamebadilisha sehem kubwa sana ya mimi mwenyewe ninavyoishi. Tukio la kwanza ambalo watu wote wanafahamu kwqamba huyu jamaa lilimtokea na amelimaliza na amemalizana nalo na kila mtu analiona na analifatilia. Mimejifunza mengi sana katika hili tangu lilivyotokea, nashkuru," amesema Chidi Benz.
Msikilize zaidi hapo chini

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages