Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, May 6, 2015

INASIKITISHA: ADEBAYOR AANIKA VISA ANAVYOFANYIWA NA FAMILIA YAKE, SOMA BARUA HII ILIYOTAFSILIWA KISWAHILI HAPA.

Mshambuliaji wa Tottenham, Emmanuel Adebayor ameandika maelezo marefu kwenye akaunti yake ya Facebook kuelezea visa anavyofanyiwa na familia yake wakiwemo mama, kaka na dada zake.
emmanuel-adebayor
Adebayor anawashutumu ndugu zake kwa tamaa ya mali zake. Licha ya kuwafanyia mambo mengi ikiwemo kuwajenga nyumba, kuwanunulia magari na kuwapa mitaji ya biashara, wameendelea kumtupia shutuma nyingi. Tumeitafsiri post hiyo kwaajili yako. Isome hapo chini.
SEA, nimezihifadhi habari hizi kwa muda mrefu lakini nadhani leo ni muhimu kuziweka wazi baadhi yake kwenu.
Ni kweli masuala ya kifamilia yanapaswa kusuluhishwa ndani kwa ndani na sio hadharani lakini nafanya hivi ili pengine familia zote zinaweza kujifunza kutokana na kile kilichotokea kwangu.
Pia weka akilini kuwa hakuna chochote kati ya haya kinahusiana na pesa.
Nikiwa na miaka 17, kwa mishahara yangu kama mcheza soka, nilijenga nyumba kwaajili ya familia yangu na kuhakikisha kuwa wapo salama. Kama nyote mnavyojua, nilishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2008. Nilimpandisha pia mama yangu jukwaani kumshukuru kwa kila kitu.
11188277_1650071258554893_8763760385803091078_n
Katika mwaka huo huo, nilimleta London kwaajili ya kufanyiwa vipimo mbalimbali. Baada ya mtoto wangu wa kike kuzaliwa, tuliwasiliana na mama yangu kumjulisha lakini muda mfupi alikataa simu na hakutaka kujua chochote.
Nikisoma maoni yenu ya hivi karibuni, baadhi ya watu walisema mimi na familia yangu tungemtafuta T.B Joshua. Mwaka 2013, nilimpa mama yangu fedha ili amtafute (Joshua) nchini Nigeria.
Alitakiwa kukaa kwa wiki; lakini simu mbili akiwa huko, nilipigiwa simu kuwa ameondoka. Pamoja na yote hayo, nilimpa mama yangu fedha nyingi kuanzisha biashara ya ‘cookies’ (vyakula vyenye sukari), na bidhaa zingine. Kwa kawaida, niliwaruhusu waziwekee jina na picha yangu ili wauze zaidi. Nini kingine mtoto wa kiume anaweza kukifanya kuisaidia familia yake?
Miaka kadhaa iliyopita, nilinunua nyumba kubwa huko East Lagon (Ghana) kwa dola milioni 1.2. niliona ni kawaida kumuacha dada yangu, Yabo Adebayor kukaa kwenye nyumba hiyo. Pia nilimruhusu kaka yangu (half brother) Daniel, kukaa kwenye nyumba hiyo. Miezi michache baadaye, nilikuwa mapumzikoni na nikaamua kwenda kwenye nyumba hiyo. Cha kushangaza, niliona magari mengi getini. Dada yangu aliamua kuipangisha nyumba ile pasipo mimi kufahamu. Pia alimfukuza Daniel kwenye nyumba hiyo. Kumbuka kuwa nyumba hiyo ilikuwa na vyumba 15.
Nilipompigia kutaka kupewa maelezo, alitumia takriban dakika 30 kunitukana kwenye simu. Nilimpigia mama yangu kumwelezea hali hiyo na yeye pia alifanya kile kile alichokifanya mama yangu. Dada huyu huyu anasema mimi sina shukrani. Muulize kuhusu gari anayoendesha ama chochote anachouza leo?
Kaka yangu Kola Adebayor, amekuwa akiishi Ujerumani kwa miaka 25. Alisafiri kurudi nyumbani kwa takriban mara nne, kwa gharama zangu. Ninalipia gharama za shule za watoto wake kila kitu. Nilipokuwa Monaco, alikuja kwangu na kuniomba hela ya kuanzisha biashara. Mungu ndiye anayejua ni kiasi gani nilimpatia. Iko wapi hiyo biashara leo hii?
Baada ya kaka yetu Peter kufariki, nilimtumia Kola kiasi kikubwa cha fedha ili aende nyumbani. Hakutokea kwenye mazishi. Na leo kaka yangu huyo huyo (Kola) anawaambia watu kuwa nilihusika kwenye kifo cha Peter.
Kivipi? Ndio kaka yule yule aliyeendenda kuongea habari za uongo kuhusu familia yetu kwenye gazeti la “The Sun” ili kujipatia pesa. Pia walituma barua kwenye klabu yangu wakati nipo Madrid ili nifukuzwe.
Nilipokuwa Monaco nilidhani ingekuwa vyema kuwa na familia ya wacheza soka. Hivyo nilihakikisha mdogo wangu Rotimi anapata chuo cha football nchini Ufaransa. Ndani ya miezi michache tu; kati ya wachezaji 27, aliiba simu 21!
Sitaweza kusema chochote kuhusu kaka yangu Peter Adebayor kwa sababu hayupo hapa leo. Roho yake ilale mahala pema peponi.
Dada yangu, Lucia Adebayor huendelea kuwaambia watu kuwa baba yangu aliniambia nimlete Ulaya. Lakini nini itakuwa sababu ya kumleta Ulaya? Kila mtu yuko hapa kwa sababu.
Nilikuwa Ghana nilipopewa taarifa kuhusu kaka yangu Peter kuwa mgonjwa mahututi. Niliendesha gari haraka iwezekanavyo hadi Togo ili kukutana naye na kusaidia. Nilipofika, mama yangu alisema nisingeweza kumuona, na nilitakiwa kuwapa tu fedha na angefanya kila kitu.
Ni Mungu tu ndio anayejua nilimpa kiasi gani siku hiyo. Watu wanasema sikufanya chochote kumsaidia kaka yangu, Peter. Mimi ni mjinga kuendesha gari kwa masaa mawili hadi Togo bure?
Niliitisha mkutano mwaka 2005 kusuluhisha masuala yetu ya kifamilia. Nilipowauliza kuhusu maoni yao, walisema natakiwa kumjengea nyumba kila mtu kwenye familia na kuwapa kila mmoja mshahara wa mwezi!
Leo bado nipo hai na wameshagawana kila mali yangu, kama ikitokea nimekufa.
Kwa sababu zote hizi, ilinichukua muda mrefu sana kuanzisha taasisi yangu barani Afrika. Kila muda nikitaka kuwasaidia watu wenye shida, walikuwa wakiniuliza maswali na wote walidhani ni wazo baya.
Kama naandika hiki, dhumuni halisi si kuwaanika watu wa familia yangu. Ninataka familia zingine zijifunze kutokana na hili.
Asanteni.

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages