Featured Posts

test

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, May 19, 2015

SAUTI SOL WATAJWA KUWANIA TUZO ZA BET MWAKA 2015. TAZAMA ALICHOKISEMA DIAMOND


Kundi la Kenya, Sauti Sol limetajwa kuwania tuzo za BET mwaka huu.

Wasanii hao wametajwa kuwania kipengele cha BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA ambacho mwaka jana Diamond alitajwa. Hakuna msanii mwingine wa Afrika Mashariki aliyetajwa kuwania tuzo hizo.
Diamond na AY ni miongoni mwa wasanii waliowapongeza Sauti Sol.
“Nawapongeza sana ndugu zangu wa Sauti Sol wa Kenya kwa kuchaguliwa kwenye tuzo za mwaka huu za BET kwenye kipengele cha BEST INTERNATIONAL ACT: AFRICA. Naamini tuzo hii inakuja Afrika Mashariki kama tukiungana na kuwapigia kura kwa wingi,” ameandika AY kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Naye Diamond ameandika: S/O to my Brothers @sautisol for the BET Nomination…. trust me! this awards is coming to East now!! Mwenyez Mungu tusmamie.”
Sauti Sol watachuana na wasanii wafuatao kwenye kipengele hicho:
AKA (SOUTH AFRICA)
FALLY IPUPA (DR CONGO)
SARKODIE (GHANA)
SAUTI SOL (KENYA)
STONEBWOY (GHANA)
THE SOIL (SOUTH AFRICA)
WIZKID (NIGERIA)
YEMI ALADE (NIGERIA)

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages