Breaking

Post Top Ad

Saturday, October 12, 2013

BAADA YA LULU KUMSIFIA JOKATE INSTAGRAM HIVI NDIVYO WATU WALIVYOMPONDA NAKUDAI KUWA ANAMPIGA VIJEMBE WEMA


Baada ya mwanadada Elizabeth Michael aka LULU kuweka hisia zake za moyoni jana kupitia mtandao mmoja wa kijamii kuhusu uzuri wa mwanadada JOKATE mwegelo kuwa “she is extra beautiful” (TAZAMA PICHA)  na yuko vizuri ile mbaya kwa urembo wananchi wenye “hasira kali” ambao bado hatujaelewa hasira zao zimetokea wapi waliamua kuandika haya yafuatayo baada ya kauli hiyo ya LULU kwa Jokate.
Wa kwanza alisema: “Anampiga vijembe wema, mtoto mswazi sana huyu”
Wa pili akafuata: “Mnafiki kweli mi nishamjua siku hizi hanipi shida”
Wa tatu akaongezea :”Jokate yote tisa, kumi jihadhari na huyu binti, ana elementi za kupindua mabwana za watu, atatembea na boyfriend wako mchana kweupee, mark my word”, alisisitza mwananchi huyu
Mwingine naye aliongezea: “Ukimuona yuko innocent lakini mmmh, nasikia…(MATENDO YANAYOKATAZWA NA JAMII) ndio jadi yao katika familia yao”
Mwingine naye alioandika: “Ila lulu mnafiki maana Wema alikuwa anamuita dada, leo anamsifia Jokate Makubwa…”
Lakini kuna watu wachache wenye uungwana na busara ambao hawakuwaunga mkono hao hapo juu ambao mmoja wao aliandika…
“Khaa! Jamani hayo mengine hayahusiani kabisaa…kaongelea uzuri hajaongelea mangine…lo, ebu achene uswahili, wabongo mmekalia unafiki sana…waacaheni wapendane…kama huwapendi haina haja ya kucomment…(TUSI) (TUSI) Zenu..”
Hatujaelewa kwanini hao wananchi wameamua kumponda sana LULU kwa mambo ambayo hayana hata uhusiano na kitu alichokipost kwenye picha.
Watanzania!!! , Je huu ni uungwana jamani, au ni kosa mtu kumsifia mwenzake?

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages