Breaking

Post Top Ad

Sunday, October 13, 2013

BREAKING NEWS: MWANDISHI WA HABARI WA ITV&RADIO ONE UFOO SARO AMEPIGWA RISASI HUKU MAMA YAKE MZAZI NAYE AKIPIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO.

TAARIFA HII KUTOKA:  RUBEN MCHOME BLOG


Taarifa za kusikitisha ambazo tumezipata hivi punde zinasema mtu mmoja anayedhaniwa kuwa mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na Radio One Ufoo Saro amefanya mauaji ya kutisha na yeye mwenyewe kujiua.
akizungumza na mtandao huu kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi umoja wa mataifa UN huko sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa)
Kamanda Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi wa Ufoo Saro(mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
TAARIFA ZAIDI NA PICHA ZA TUKIO ZITAKUJIA HIVI PUNDE

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages