Breaking

Post Top Ad

Monday, May 25, 2015

DESIGNER WA CHRISBROWN NA AUGUST ALSINA UMUUMBUA DIAMOND KWA KUVAA NGUO ZAKE FEKI. ALETA FUJO INSTAGRAM

Kuna usemi usemao kuwa ‘wagombanao ndio wapatanao’ na hiki ndicho kilichotokea weekend hii.
11280524_1591248307791375_1969743305_n
Diamond akiwa amevaa nguo ya Roperrope ambayo designer wake mmarekani alidai kuwa ni feki
Devontae Roper, ni designer wa Los Angeles, California, Marekani ambaye ametokea kujipatia umaarufu kwa nguo zake zinazovaliwa na mastaa wa muziki nchini humo wakiwemo August Alsina, YG, Chris Brown, Future na wengine. Brand yake inajulikana kwa jina la RoperRope.
10932480_1526213564327356_1789732294_n
Devontae Roper
Juzi Roper alipost picha ya Diamond Platnumz akiwa amevaa nguo zenye mfanano na designs zake na kumchana staa huyo kuwa ameiba ubunifu wake kupitia yule Diamond aliyemuita kama ‘designer’ wake ambaye kazi yake hasa ni ‘stylist’.
11055930_581514308619035_171918323_n
“I usually don’t blast people who make or wear fakes of my designs but this person went way too far when they used my logo! @diamondplatnumz is wearing fake #Roperrope shirt made by a person with bad character and a strong lack or originality! This is not ok! If you steal a design please reframe from using the Designers Logo because it’s illegal www.shoproperrope.com,” aliandika kwenye Instagram.
Post hiyo ambayo hata hivyo tayari imefutwa ilisababisha mjadala mkubwa na wengi iliwafanya wamfahamu Roper ambaye nguo zake zimekuwa zikionekana kwenye video nyingi za August Alsina, Future na Chris Brown.

Wapo waliomshutumu Diamond na kudai kuwa ameumbuka lakini wengi walimtetea na kwa kusema yeye ni mvaaji tu wa nguo hizo na hana kosa hata kama alivaa nguo feki.

Roper alipost picha nyingine ya Diamond na kuandika: Bless Up emoji I just got news #Roperrope just went International emoji God is everywhere #YoungGod x #ICantLose #ShippingOverseas #ThanksEastAfrica #GodFlow @DiamondPlatnumz hit me up next time.”

Post Top Ad

Pages