Breaking

Post Top Ad

Tuesday, May 26, 2015

KAJALA: MPAKA NA KUFA SITOMSAHAU WEMA NA PETIT. SOMA SABABU HAPA.

Licha ya kuwa urafiki wa muigizaji Kajala Masanja na Wema Sepetu bado uko juu ya mawe, lakini muigizaji huyo amesema kuwa mpaka siku anaenda kaburini hawezi kusahau wema aliofanyiwa na Wema pamoja na Petit katika kipindi alichokuwa na matatizo.
11283318_552779328195720_588926409_n
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Kajala ameandika ujumbe mrefu wa kuelezea jinsi ambavyo hawezi kuwasahau Wema na Petit waliokuwa nae bega kwa bega katika kipindi kigumu alichopitia.
Wema na Petit
“BINADAMU TULIUMBWA KUISHI KATIKA MISINGI YA UBINADAMU NA SIO UNYAMA KAMA WAISHIVYO WANYAMA WA PORINI LEO NAOMBA KUSEMA KUTOKA MOYONI MWANGU.. NAJUA KABISA NINA WAZAZI WANGU NDUGU ZANGU NA ZAIDI SANA MUNGU WANGU ILA KUNA WATU MPAKA NAKUFA KAMWE SINTOWASAHAU KATIKA KUTA ZA MOYO WANGU KATIKA KIPINDI CHANGU KIGUMU NILICHOPITIA MLIKUWA NEMBO NAMBONI KUBWA KATIKA KUOKOA MAISHA YANGU… NAPENDA KUSEMA KUWA HATA KWA HAYA YOTE TUNAYOPITIA BADO NI MADOGO SANA KUFICHA THAMANI YENU MLIYOIJENGA JUU YANGU..NAKUMBUKA SANA MLIPOJITOA KWA AJILI YANGU MLIPOJINYIMA KWA AJILI YANGU MLIPOPIGANA KWA AJILI YANGU,MLIVYOFEDHEHEKA KWA AJILI YANGU YOTE HAYO NAYAKUMBUKA NA NAMSHUKURUU MUNGU KWANI NAONA KABISA MLILETWA DUNIANI KWA SABABU NYINGI NA MOJA YA SABABU ILIKUWA KUNIOKOA KATIKA KIPINDI KIGUMU KATIKA MAISHA YANGU.LEO HII TAREHE 25.5.2015 NAPENDA KUSEMA KWA UMMA NA ZAIDI KWA MUNGU WANGU KUWA NAWATHAMINI NAWAPENDA NA NASHUKURUUU SANA KWA YOTE MLIYOFANYA JUU YANGU.. NAWAOMBEA KWA MUNGU MUENDELEE NA MOYO HUO HUO KWANI NAAMINI KUNA WENGI BADO WANAWATEGEMEA ILI KUKOMBOA MAISHA YAO KWA WAKATI ALIYOPANGA MUNGU
HATA KITABU CHA DINI KILISEMA KUWA “huwezi kumpenda Mungu usiyemuona wakati unamchukia ndugu yako unayemuona” NAJUA SIKU MOJA TUTAISHI KAMA ZAMANI.. AHSANTENI.”
Hivi karibuni Kajala akiongea na Amplifaya alisema kuwa mpaka sasa yeye na Wema hawaongei, na hakuna mtu anayeweza kuwapatanisha hadi pale wao wenyewe watakapojikuta tu wamekutana na kuyamaliza.
“Mi nadhani kupatana mimi na Wema tutapana Mungu akipenda, lakini watu waseme ooh mimi hapa nimekuja nawapatanisha hiyo haitasaidia, Wema akiskia moyo wake unataka kuongea na Kajala na Kajala akijiskia yah tukikutana tutajikuta tu wenyewe tunaongea tutayamaliza.”

Post Top Ad

Pages