Breaking

Post Top Ad

Friday, May 22, 2015

PICHA ZA LULU MICHAEL AKIWA MJAMZITO ZAWASHTUA WENGI, SOMA STORI KAMILI HAPA.


 

Staa mwenye historia ya kuingia kwenye tasnia ya uigizaji Bongo akiwa na umri mdogo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Chanzo cha habari kimeeleza kwamba, mwigizaji huyo kwa sasa ana zaidi ya miezi mitatu akiwa anajificha baada ya madai hayo ya kunasa ujauzito ambao umekuwa ukimpeleka puta kiasi cha kushindwa kutimiza majukumu yake kama ilivyokuwa awali.
Staa mwenye historia ya kuingia kwenye tasnia ya uigizaji Bongo akiwa na umri mdogo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anadaiwa kuishi kwa kujificha kufuatia madai kwamba huenda mimba yake imekua kubwa hivyo inamfanya kuwa hoi na kushindwa kuendelea na misele ya kazi za sanaa.
Ilidaiwa kwamba, kufuatia hali hiyo, mwanadada huyo hata mahudhurio yake chuoni (Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar) huku akitupia mtandaoni picha za pasipoti (za uso) na kuficha sehemu zingine za mwili.

“Najua itakuwa ngumu sana kuniamini moja kwa moja ila ukweli ni kwamba, kwa sasa Lulu amekuwa mtu wa kujificha, hawezi hata kutoka nyumbani kwa sababu ya ujauzito.“Hata kujichanganya kwenye shughuli za Bongo Movies na wenzake siku hizi haonekani,” kilidai chanzo hicho na kuongeza kuwa hata kwenye Shindano la TMT (Tanzania Movie Talents), Lulu haonekani kama mwaka jana.
Baada ya kupata ubuyu huo, paparazi wetu alimtafuta Lulu ili wakutane uso kwa macho aweze kujiridhisha juu ya madai hayo lakini zoezi hilo lilishindikana hivyo aliamua kuzungumza naye kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alipopatikana alielezewa madai yote kisha akafunguka:
“Ni kweli kuna vitu kwa sasa sivifanyi ila si kwa sababu ya mimba.
“Najua kila mtu anaongea anachojisikia, suala la kuposti picha za nusu mwili, kweli nalifanya sema mimba ni jambo la kheri isiwe dili kwa sababu iko kwangu tu.

“Hata ishu za chuo mimi ninaenda ingawa si kila siku maana kila kitu kina mipangilio yake.
“TMT mimi nipo, nafikiri watu wafuatilie tu mwisho wa siku wataniona maana haya mambo yote ni ‘surprise’. Kama mimba ipo watu wataiona tu ikikua maana kuna mahali tutakutana na hata nikifanikiwa kuificha sana, mtoto hawezi kufichika, mashabiki waendelee kusubiria surprise kutoka kwangu.


Elizabeth Michael ‘Lulu’. “Katika maisha yetu Waafrika si lazima kila jambo lifahamike waziwazi, naomba ieleweke hivyo, maana kuzaa natamani leo hata kesho kwa kuwa mimi sasa ni mtu mzima na niko tayari kuzaa tena kwa umri huu nilionao.”
Kwa muda wa miezi kadhaa mitandao ya kijamii imekuwa ikiripoti juu ya madai ya Lulu kuwa mjamzito bila mwenyewe kuthibitisha

Post Top Ad

Pages