Breaking

Post Top Ad

Thursday, June 4, 2015

MSIKILIZE LINAH AKIONGEA KUHUSU WEMA KUTEMBEA NA EX WAKE, TEAM WEMA WAENDELEA KUMCHAMBA LINAH.

Linah Sanga amesema taarifa kuhusu uhusiano kati ya Wema Sepetu na aliyekuwa mpenzi wake umemshangaza.


Akiongea kwenye kipindi cha Ala za roho cha Clouds FM, Linah alisema yeye na mpenzi wake waliachana rasmi miezi miwili iliyopita.
“Hata mimi nasikia kuwa sasa hivi anatoka kimapenzi na Wema Sepetu,” alisema Linah. “Unajua mtu kama alishawahi kuwa mtu wako lazima upate mshtuko, kwakweli hata mimi imenishtua sana. Kwahiyo mimi namuachia Mungu, nina imani aliyopanga Mungu binadamu hawezi kupangua. Na pia nawatakia kila lakheri katika mahusiano yao. Sasa hivi nipo busy na kazi zangu maana mimi sikuzaliwa naye na wala sitozikwa naye. Na mimi kwa upande wangu nipo poa kabisa.”
Msikilize zaidi Linah hapo chini.

Post Top Ad

Pages