Breaking

Post Top Ad

Sunday, July 19, 2015

ALICHOKISEMA DIAMOND BAADA YA KUSHINDA TUZO ZA MTVMAMA 2015 "BEST LIVE ACT"

11199470_1002922379731138_968098397_nMuimbaji huyo ambaye pia alidondosha show ya kukata na shoka kwenye tuzo hizo akiwa na msanii wa Nigeria, Flavour na kuimba hit yao, Nana, amewashukuru watanzania na wengine waliomwezesha kushinda tuzo hiyo.
“Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote #TeamWasafi kwa kunipigia kura na Kuhamasisha kwa Nguvu,” ameandika kwenye Instagram.
“Niushkuru sana Uongozi wangu, Familia pamoja na Team nzima ya @wcb_wasafi hususan Madancers wangu kwani Naamini wao ndio wamenipika nikapikika hadi leo hii kuweza kuletaTunzo hii Nzito ya Mtumbwizaji Bora Africa, Nyumbani…lakini pia Shukrani za kipekee zimfikie Mama yangu kipenzi Sandra kwa Mafunzo na Malezi anayonipa kila siku juu ya Dunia,” ameongeza.
“Na Shukran tena za kipekee na aina yake zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu @zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa M’bunifu kwenye kazi..emoji #BestLiveAct #Mtvmama2015 Asanteni sana.”

Post Top Ad

Pages