Breaking

Post Top Ad

Tuesday, June 27, 2017

BET AWARDS 2017: HAWA NDIO WASHINDI WA TUZO ZA BET - BEYONCE, REMY MA, CHANCE THE RAPPER..

Usiku wa kuamkia leo kulikuwa na sherehe za ugawaji wa tuzo za BET jijini Los Angeles nchini Marekani, Tuzo ambazo watu wengi walikuwa wakisubiria kwa hamu kujua mshindi wa kipegele cha Best Female Hip-Hop Artist ambapo kulikuwa na majina makubwa kama Nicki Minaj, Remy Ma,Cardi B Missy Elliott na Young M.A ambapo Remy Ma ameibuka mshindi na kumnyamazisha hasimu wake Nicki Minaj.
2017 BET Awards - Show
Remy Ma
Washindi wengine ni mama wa mapacha wawili, Beyonce ambaye ameibuka na tuzo 5 kutoka kwenye vipengele vya Muimbaji bora wa kike wa RnB/Pop, Album bora ya mwaka (Lemonade), Video bora ya mwaka (Sorry) , Muonozaji bora wa video wa mwaka ambapo tuzo wamegawana na Kahlil Joseph kupitia video ya wimbo wa (Sorry) na tuzo yake ya tano kachukua kwenye kipengele cha Viewers’ Choice Award .

Chance The Rapper
Msanii mwingine aliyeibuka kidedea kwa kukwara tuzo nyingi ni Chance The Rapper ameibuka na Tuzo tatu kutoka kwenye vipengele vya Best New Artist,Best Collaboration ambapo ngoma yake ya ‘No Problem’ aliyomshirikisha 2 Chainz ndiyo imechukua tuzo na kipengele cha  Humanitarian Award tuzo hii ya heshima amepewa baada ya kutoa misaada kwenye shule za umma huko Chicago.
Wasanii wengine walioshinda tuzo usiku wa jana ni Bruno Mars, Kendrick Lamar, Solange,Mchezaji wa Kikapu Steven Curry na mcheza tenesi Serena Williams.
Tazama Orodha kamili ya washindi wa tuzo za BET hapa chini.
 • Best Female R&B/Pop Artist: Beyonce Knowles
 • Best Male R&B/Pop Artist: Bruno Mars
 • Viewer’s Choice Award: Beyonce Knowles, “Sorry”
 • Best Group: Migos
 • Best Collaboration: Chance the Rapper Ft. 2 Chainz, “No Problem”
 • Best Male Hip-Hop Artist: Kendrick Lamar
 • Best Female Hip-Hop Artist: Remy Ma
 • Video of the Year: Beyonce Knowles, “Sorry”
 • Video Director of the Year: Kahlil Joseph and Beyonce Knowles – “Sorry”
 • Best New Artist: Chance the Rapper
 • Best Actress: Taraji P. Henson
 • Best Actor: Mahershala Ali
 • Dr. Bobby Jones Best Gospel/Inspirational Award: Lecrae, “Can’t Stop Me Now (Destination)”
 • Youngstars Award: Yara Shahidi
 • Best Movie: “Hidden Figures
 • Sportsman of the Year: Stephen Curry (II)
 • Centric Award: Solange Knowles, “Cranes in the Sky”
 • Album of the Year: Beyonce Knowles, “Lemonade”
 • Best International Act Europe: Stormzy
 • Best International Act Africa: Wizkid
 • Humanitarian Award: Chance the Rapper
 • Lifetime Achievement Award: New Edition
SOURCE: Bongo 5

Post Top Ad

Pages