WEMA AMZUNGUMZIA DIAMOND NA ZARI,.. SOMA HAPA STORI KAMILI.

0 comments
MISS Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Akizungumza na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema Diamond huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.

Wema alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Diamond ili kila mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.

SAFARI YAKE CHINA NAYO TATIZO
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake,
Wema alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Diamond hakutaka asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.

MWISHO WA LIKIZO
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28  kama ilivyo
kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Diamond.

AMZUNGUMZIA ZARI
Staa huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi na Diamond, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana ‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.

BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
“Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi,” alisema Wema.

DIAMOND AULIZWA KAMA ANAITAMBUA LIKIZO NDEFU
Baada ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Diamond kwa lengo la kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.

“Nashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,” alisema Diamond huku akichekacheka kwa ishara ya furaha akijiandaa kuachia ngoma kali mpya iitwayo ‘Nitampata Wapi’ leo.

KWENYE WHATSAPP
Wakati Diamond akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”

Wema na Diamond wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.Read More »

NEW AUDIO: DIAMOND PLATNUMZ - NTAMPATA WAPI. DOWNLOAD HERE

0 comments


Read More »

ALICHOKISEMA DIAMOND PLATNUMZ NDANI YA "LEO TENA" KAMA WAMEACHANA NA WEMA AU LAAH!!. SOMA HAPA.

0 comments
Wakati akiachia ngoma yake mpya ‘Ntampata Wapi’, Diamond Platnumz ameendelea kuteka vichwa vya habari kuhusiana na tetesi kuwa wameachana tena na mpenzi wake, Wema Sepetu.
wpid-wema-akiwa-pembeni-kumsupport-diamond1.jpg
Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM leo, Diamond alionekana kutokuwa tayari kuzungumza ukweli wa jambo hilo licha ya watangazaji wa kipindi hicho kumbana.
“Kuna vitu fulani vinapokuja kuhusu mapenzi sometimes inakuwa sio vizuri kuvi.. kuna vingine vinafaa kwenda kwenye media, vingine vinakuwa havifai,” amesema.
“Kuna kitu unaniuliza nashindwa kukiongea straight kwasababu hakijafika wakati wa kwenda kwenye media so kuzungumza inaweza ikatengeneza maana mbaya. Vitu vingi sana vinaandikwa, navisoma lakini mimi na yeye ndio tunaujua ukweli uko wapi. Ikifika muda wa kuweka wazi tutaweka wazi.”

Read More »

NEW VIDEO: DIAMOND PLATNUMZ - NITAMPATA WAPI. DOWNLOAD HERE.

0 comments

Read More »

HUYU NDIYE MTOTO"MTAALAMU WA IT" MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE DUNIANI.

0 comments


Ayan Qureshi.
Ayan Qureshi.
Wazazi wengi Afrika wamekuwa hawajali kuvitambua vipaji vya watoto wao kipindi wanapokua kwenye hatua ya utoto na wanapoanza kukua, mfano mzuri ni kwamba ukiongea na watu ambao wana vipaji na uwezo mkubwa kwenye mchezo kama mpira wa miguu, ama kuimba na vinginevyo utagundua kwamba jitihada binafsi zimewaongoza kugundua vipaji vyao na mchango wa wazazi ni mdogo ama usiwepo kabisa.
Hot news kutoka Coventry, Uingereza inamhusu Ayan Qureshi ambaye ana umri wa miaka sita tu, na mwaka jana aliingia kwenye list ya watoto waliofanya maajabu ambapo alifanya mtihani wa kampuni ya Microsoft unaothibitisha wataalamu wa IT duniani na kufaulu, baba yake ambaye ni mtaalamu wa IT anasema alimfundisha mtoto wake kuhusu masuala ya Kompyuta tangu akiwa ana umri wa miaka mitatu.
Katika mahojiano na mtoto huyo amesema mtihani ulikuwa mgumu lakini alienjoy kuufanya na alijiandaa kwa miezi mingi kabla ya kuufanya, kutokana na kufaulu mtihani huo kwa sasa anakuwa ni mtaalamu wa IT aliyethibitishwa na Microsoft ambaye ana umri mdogo zaidi duniani.
Hiki ndicho cheti alichopewa mtoto huyo na Kampuni ya Microsoft.
Hiki ndicho cheti alichopewa mtoto huyo na Kampuni ya Microsoft.
 Hii ni video ya mtoto huyo iliyopo kwenye mtandao wa Youtube, unaweza kuitazama hapa.
 

Read More »

VIDEO: TAZAMA INTERVIEW HII LAVEDA A. AZUNGUMZIA ISHU YA KUJICHUA.

0 comments

Read More »

NEW SONG : MWASITI FT KING ZILLAH - LEO . DOWNLOAD HERE

0 comments

Read More »

KWA MANENO HAYA YA WEMA SEPETU INSTAGRAM!! LAZIMA ATAKUWA AMEACHANA NA DIAMOND

0 comments

Read More »

linkwithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...